((Na Mwenyezi Mungu hakuwapoteza watu baada ya kuwa amewaongoa mpaka awabainishie wanayopaswa kujiepusha nayo. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu.))
Katika Sura Ibrahim: ((Na hatukumtuma Mtume ila kwa lugha ya kaumu yake ili awabainishie. Kisha Mwenyezi Mungu humpoteza amtakaye na humuongoa amtakaye. Naye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hikima.)) Katika Surat Al-Qiyamah: “Basi ni juu Yetu kuifafanua.” Na katika Surat At-Tawbah: “Na Mwenyezi Mungu hakuwapoteza watu baada ya kuwa amewaongoa mpaka awabainishie wanayopaswa kujiepusha nayo. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu. Katika Surat Al-Isra’: “Mwenye kuongoka basi ameongoka kwa ajili ya nafsi yake, na anaye potea basi amepotea kwa hasara yake, na wala habebi mzigo wa mwingine, na wala Sisi hatuadhibu mpaka tumpeleke Mtume. Ni wale tu waliosoma kitabu changu, Jumbe Zinazongojewa, na wakaelewa yaliyomo ndani yake ndio watakaozitafakari Aya hizi, ili wapate kujua hali ya watu itakapodhihiri Mahdi huko mbeleni, na Mwenyezi Mungu ndiye anajua zaidi.